Na’feel kama fala
Kukam kukuambia hili
Unaona ule kiangazi?
Mwenye amezubaa chini ya jua?
Hali inasema atakam kukupora
Atakupora green yako
Wewe na wana wako
Akapandishia joto na kuiba maji kwa miguu yako
Slowly utakufa,
Na ukikufa,
Wenzako watakufa
Wanyama including man hata
Africa ndio itaanza
Juu nchi si za kwanza, wala pili, ni za tatu
Infrastructure na technolojia hazina katu
Wataangaika watu
Juu ni sisi tuliunda viwanda vya coal na kuchoma miti ya makaa
Tukaacha ozone ikae vile inakaa
Ku’ignore sea level ya pwani ilipopanda
Victoria na Turkana ziki’flood kujifanya ma’danda
Sijitetei, niko hapa ku’acknowledge blunder
Na kukuahidi hakuna kiangazi tena itakuja
Hakuna kampuni itajificha kwa siasa kutuvunja
Tunakuja kuhakikisha coal imebaki kwa mchanga
Yajayo tunaganga
Tunakam tuki’match kwa barabara
Wooola!
Sisi ni vijiji zimewashwa na solar
Michanga freshi ukisorora
Jeshi ya mayut wako kwa ma’bicycle
Zaidi ya ku’re – use tuna’recycle
Fear haikoo
Tunapunguza safari za ndege
Bahari
Na Gari
Na kama Lazima Gari, basi za stima
Ima fa Ima
Kukata plastiki
Kupanda miti
Kuunda kujenga
Wasanii malenga
Kuchora kuandika
Tuta’spread na kwa uhakika neno litafika

Usiku ukifika
Funga macho
Pumua
Hatutakuangusha
Utaona.

By Lexas Mshairi

 

53 Comments

Leave a Reply